You are currently viewing USALAMA WA WATOTO MTANDAONI

USALAMA WA WATOTO MTANDAONI

Na Martin Kedenge
Teknolojia na matumizi ya mtandao nchini ya mekuwa kwa silimia kubwa huku
watumizi wakiendele kuongezeka kila uchao. Kulingana na shirika la muungano
wa kimataifa wa mawasiliano ITU, mwaka wa 2019 taifa hili liliandikisha idadi
ya wakenya million arobaini na sita laki nane na sabini mia nne na ishirini na
mbili wanaotumia mtandao.Takwimu hizo bado hazijadhibitishwa na tume ya
mawasiliano nchini CAK japo mikakati imewekwa kuzibainisha. Ni ishara
tosha kuwa wakenya wanategemea mtandao kwa shughuli zao za kila siku.
Sehemu za kutumia mitandao zinaendelea kufunguliwa maeneo mbalimbali
nchini huku kila nyumba ikijitahidi kununua simu ambayo inasaidia kutekeleza
shughuli mtandaoni. Hali hii imesababisha Watoto kutambulishwa katika
matumizi ya mtandao hasa kwa wale waliofanikiwa kupata nafasi ya kumiliki
vifaa hivyo.
Kutokana na idadi kubwa ya Watoto wanaotumia mitandao kote duniani,
Muungano wa kimataifa wa mawasiliano ulianzisha mradi wa kubuni mbinu ya
kuwalinda Watoto mtandaoni dhidi ya madhara yanayotokana na habari potovu.
Hatua hiyo imeonekana kukumbatiwa na mataifa mbalimbali Kenya ikiwa
miongoni mwake.
Mwaka wa 2014 Mamlaka ya mawasiliano nchini CAK iliamua kuanzisha
mradi huo nchini wa Be the COP ili kuwalinda Watoto dhidi ya hatari
zinazotokana na matumizi ya mtandao.Mradi huo ambao unaendelea
unatazamia kutoa habari kuhusu namna ya kuwalinda Watoto wanapotumia
mitandao na kuhakikisha wako salama. Mamlaka hiyo hiyo imeshirikiana na
washikadau mbalimbali katika harakati za kufanikisha kampeini hiyo kote
nchini. Iwapo kampeini hiyo itakumbatiwa na kila mkenya, basi idadi kubwa ya
Watoto nchini italindwa dhidi ya hatari za mtandaoni kwani kufikia sasa shule
nyingi nchini zinatumia teknolojia katika masomo.
Kufungu cha 29(D) cha katiba ya Kenya kinasema kuwa kila mtu ana haki ya
uhuru na usalama ambayo ni pamoja na haki ya kutokuteswa kwa njia yoyote
ile, iwe ya mwili au ya kisaikolojia. Pia kifungu cha 46(C) juu ya ulinzi wa
watumiaji inasema kwamba watumiaji wana haki ya kulindwa afya zao,
usalama na masilahi ya kiuchumi.

Sheria ya Watoto Nambari 8 ya 2001 inapeana jukumu la uwajibikaji wa
wazazi, kukuza,kulinda,kutunza na kuelekeza Watoto. Kifungu hiki
kinawalinda Watoto dhidi ya matumizi ya mitandao pia.

Leave a Reply